Home Ligi Kuu DIDA: BADO TUNA NAFASI YA KUBAKI NDANI YA LIGI

DIDA: BADO TUNA NAFASI YA KUBAKI NDANI YA LIGI


 KIPA namba moja wa kikosi cha Ihefu ya Mbeya kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila, Deogratius Munish, ‘Dida’ amesema kuwa ikiwa wataongeza juhudi timu hiyo itabaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Dida amekaa langoni kwenye mechi 9 ambazo ni dakika 810 kati ya 24 ambazo timu hiyo imecheza.

Ameokota nyavuni jumla ya mabao 15 kati ya 34 ambayo timu hiyo imefungwa ana wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 54.

Ihefu FC ipo nafasi ya 17 ina pointi 20 jambo ambalo linawafanya wawe kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa hawataongeza juhudi kusaka ushindi kwenye mechi zao zijazo.

Mkongwe huyo ambaye amepata nafasi ya kucheza pia ndani ya Yanga, Simba na Lipuli amesema kuwa bado anaamini kikosi hicho kina nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

“Ni kweli matokeo ambayo yamekuwa yakipatikana ni magumu kwetu hasa pale timu inapopoteza, lakini nina amini kwamba bado kuna nafasi ya kubaki kwenye ligi ikiwa tutaongeza juhudi.

“Yapo makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya jambo ambalo linatufanya tushindwe kupata matokeo nina amini kwamba benchi la ufundi linaona na litayafanyia kazi makosa yetu,” .

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...RUVU SHOOTING 'WAJICHUA' KWA MASAA MANNE JUANI..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here