Home Ligi Kuu IHEFU FC HAWAJAKATA TAMAA NDANI YA LIGI KUU BARA, MATUMAINI YAKUTOSHA

IHEFU FC HAWAJAKATA TAMAA NDANI YA LIGI KUU BARA, MATUMAINI YAKUTOSHA

  

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Klabu ya Ihefu FC ya Mbeya amesema kuwa bado kuna nafasi kubwa kwa timu hiyo kujinusuru kwenye janga la kushuka daraja licha ya kuwa na mwendo wa kusuasa.

Katwila aliibuka ndani ya Ihefu FC akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.

Kikosi chake kikiwa kimecheza jumla ya mechi 24 kimekusanya pointi 20 kipo nafasi ya 17 huku Mwadui FC ikiwa na pointi 16 nayo imecheza mechi 24 ipo nafasi ya 18.

Katwila amesema kuwa bado kuna mechi ambazo zipo mkononi hizo wakipata matokeo watatoka hapo walipo.

“Ukitazama bado tuna mechi kupitia hizonina amini kwamba ikiwa tutapata matokeo chanya basi tutakuwa na hadithi nyingine ya kusimulia hivyo bado tupo na imani yetu msimu ujao tutakuwa ndani ya ligi.
“Ikiwa tutashinda maana yake ni kwamba tutaondoka kwenye presha ya kushuka daraja, mashabiki wasikate tamaa sapoti yao ni muhimu kwani hata wachezaji nao wanazidi kupambana.

“Ushindani ni mkubwa kwa sababu kila timu ambayo inaingia uwanjani inahitaji ushindi hata sisi pia tunahitaji pointi tatu kwenye mechi zetu,” .

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO