Home Ligi Kuu JKT TANZANIA YAIPIGA MKWARA SIMBA

JKT TANZANIA YAIPIGA MKWARA SIMBA


ABDALAH Mohamed,’Bares’ Kocha Mkuu wa Klabu ya JKT Tanzania amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Mchezo wa leo ni wa mzunguko wa pili ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma dakika 90 zilikamilika JKT Tanzania 0-4 Simba.

Hivyo leo unatarajiwa kuwa mchezo wa kisasi kwa kuwa JKT Tanzania inapambana kutoshika daraja huku Simba ikipambana kuishusha Yanga nafasi ya kwanza ili kuweza kutetea ubingwa wake.

Kwenye msimamo JKT Tanzania ipo nafasi ya 10 imekusanya jumla ya pointi 24 baaada ya kucheza jumla ya mechi 21. Inakutana na Simba Uwanja wa Mkapa iliyokusanya jumla ya pointi 42 ipo nafasi ya pili na imecheza jumla ya mechi 18.

Bares amesema:”Vijana wapo vizuri na wanatambua kwamba tunacheza na timu ya aina gani, kikubwa ambacho tunahitaji ndani ya uwanja ni ushindi.

“Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwani hakuna mwalimu ambaye anapeleka timu uwanjani akiwa anafikiria kupoteza,” amesema.

Leo Bares atakosa huduma ya mtupiaji wake namba moja Adam Adam mwenye mabao 7 kwa kuwa yupo Uturuki kwa ajili ya majaribio.


SOMA NA HII  KOCHA POLISI TZ : SIMBA WAMESHINDA KWA KUBEBWA..ALIA PENALTI YA KIUJANJA UJANJA YA MORRIOSN..