Home Yanga SC KISUBI ATAJA SIRI YA KUOKOA PENALTI YA MUGALU

KISUBI ATAJA SIRI YA KUOKOA PENALTI YA MUGALU


MLINDA mlango wa kikosi cha Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi amesema kuwa, alijua kama angeokoa penalti ya mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu.

Kisubi alikuwa mwiba mkali katika mchezo wa juzi Jumatano usiku, ambapo aliweza kuisaidia Prisons kuondoka na pointi moja, baada ya kuokoa mashuti tisa ya hatari yaliyoelekezwa langoni mwake.

Katika mchezo huo Kisubi aliokoa Penalti hiyo dakika ya 29 ya mchezo baada mlinzi wa timu hiyo, Vedastus Mwihambi kuunawa mpira ndani ya eneo la 18. 

Akizungumzia penalti hiyo Kisubi amesema: “Kuhusiana na Penalti ya Mugalu, kosa kubwa alilolifanya ni kukubali kunipa mpira kabla hajaupiga, kwani ni wakati huo alitaka kuniibia na kuchungulia wapi atapiga.

“Hapohapo nilifanikiwa kung’amua ni upande gani angepiga na ndiyo maana nikafanikiwa kuicheza ile penalti,” 

Sare hiyo imewafanya Tanzania Pisons kufikisha pointi 28 na kuendelea kujiimarisha katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.

SOMA NA HII  BIGIRIMANA AENDELEA KUIKALIA KOONI YANGA...WAKALA WAKE ATUA TZ NA 'MKWARA WA KIBABE'...