Home Simba SC LUIS MIQUISSONE KWENYE VITA NYINGINE NA WABABE WA AFRIKA

LUIS MIQUISSONE KWENYE VITA NYINGINE NA WABABE WA AFRIKA


 WACHEZAJI wanne wanaocheza soka la Afrika wamechaguliwa kuingia kwenye mchakato wa kumsaka mchezaji bora wa wiki ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyota bora wa wiki iliyopita mwenye tuzo tatu ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika anayecheza ndani ya Klabu ya Simba Luis Miquissone jina lake lipo kwenye orodha akiwa kwenye vita nyingine na wababe ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo imekuwa na ushindani mkubwa.

Luis ana tuzo tatu ambazo amepewa na Caf baada ya kufanya vizuri ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ya kwanza ni ile ya bao bora ambalo aliwatungua Al Ahly, mchezaji bora wa wiki pamoja na kuwa ndani ya kikosi cha wiki.

Wengine ambao anashindana nao ni pamoja na Hamdou Elhoun wa Klabu ya Esperance, Mohamed Afsha wa Al Ahly na kipa Denis Onyango wa Mamelod Sundowns.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIWA KUANZA DHIDI YA AFRICAN LYON