Home Azam FC MASTAA AZAM WAPEWA WIKI MBILI

MASTAA AZAM WAPEWA WIKI MBILI

[the_ad id="25893"]


BENCHI la ufundi la klabu ya Azam kwa kushirikiana na uongozi wa kikosi hicho, umeamua kuwapa nyota wote wa kikosi hicho mapumziko ya wiki mbili kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa ya kirafiki.

Azam ni miongoni mwa timu ambazo zimefanikiwa kutoa nyota wengi kutoka kikosi chao cha kwanza, ambao wamekwenda kujiunga na vikosi vya timu za mataifa yao kwa ajili ya michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON.

Akizungumzia hilo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Baada ya ligi kusimama kwa muda kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa, benchi la ufundi pamoja na uongozi umeamua kuwapa mapumziko ya wiki mbili nyota wetu wote.

“Hii inamaanisha wachezaji wetu wote ikiwemo wale ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za Taifa, watakuwa na mapumziko ya wiki mbili na watarejea pamoja na wenzao waliojiunga na timu za taifa baada ya muda huo,”

SOMA NA HII  AZAM KAMILI GADO KUIVAAA TP MAZEMBE LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here