Home Azam FC MPANGO WA AZAM FC KUIONDOA YANGA KILELENI UMECHORWA HIVI

MPANGO WA AZAM FC KUIONDOA YANGA KILELENI UMECHORWA HIVI




 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utatumia mpango wao wa kutumia faida ya matokeo mabaya ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwa lengo la kuwaondoa kileleni.

Azam yenye pointi 44 wapo nyuma ya Yanga wenye 50 wakitofautiana idadi ya michezo waliyocheza yenyewe ikiwa mbele kwa 24 na wapinzani wao 23.

 

Timu hizo zote zimepania kubeba taji hilo katika msimu huu unaotetewa na Simba ambao wenyewe wapo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 46.

 

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa kabla ya kuanza kwa msimu walijiwekea malengo na kubwa ni kubeba ubingwa wa ligi msimu huu.


“Tangu mwanzoni mwa msimu huu tuliweka wazi kuwa tuna jambo letu, na hii ni katika kuhakikisha tunajitahidi kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.

 

“Hivyo, hatuna presha na mtu aliye nyuma yetu, bali sisi tunamwangalia aliye juu yetu na kwa sasa Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi, hivyo malengo yetu ni kujitahidi kushinda michezo iliyo mbele yetu ili kupunguza pengo la pointi lililo kati yetu.

 

“Uzuri ni kwamba Yanga nao hawajawa na mwendelezo mzuri na wameangusha pointi nyingi, hivyo ni jukumu letu kulichukulia hilo kama faida na kuwakaribia au hata kuwazidi.”

SOMA NA HII  AZAM FC KUENDELEA PALE WALIPOISHIA