Home Burudani BURNA BOY ASHINDA TUZO YA BET

BURNA BOY ASHINDA TUZO YA BET


Hatimaye mshindi wa tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act’, atajwa kuwa ni Burna Boy.

Burna Boy ametajwa kushinda tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo Juni 28, 2021 ambapo kilele cha utoaji tuzo hizo umefanyika, nchini Marekani.

Ushindi wa msanii huyo kutoka Nigeria, unamfanya awabwage washindani wake waliokuwa wakichuna katika kipengele hicho akiwemo Diamond Platnumz kutoka Tanzania na Wizkid kutoka nchini Nigeria.

Wengine waliokuwa katika kipengele hicho ni Aya Nakamura (Ufaransa),Emicida (Brazili), Headie One (Marekani) Young T & Bugsey (Marekani) na Youssoupha (Ufaransa)

Vilevile hii inakuwa mara ya tatu kwa Burna Boy kushinda kipengele hicho kwani alishachukua tuzo tena mwaka 2019 na 2020.

Tuzo za BET zilianza kutolewa mwaka 2001, zinazoandaliwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo, zinatolewa usiku wa leo huko nchini Marekani.

SOMA NA HII  KAMA UNA MTOTO MDOGO...HILI LA DStv LINAKUHUSU...ALADDIN INAKUJIA KWAKO KWA MSELELEKO ULE ULE WA MAMBO MOTO...