Home Uncategorized KOCHA WA NAMUNGO AWATAKA WAZAWA KUTAFUTA CHANGAMOTO MPYA NJE YA BONGO

KOCHA WA NAMUNGO AWATAKA WAZAWA KUTAFUTA CHANGAMOTO MPYA NJE YA BONGO


KOCHA Mkuu wa timu ya Namungo FC, Hitimana Thiery raia wa Burundi amesema kuwa ni muhimu kwa makocha wa bongo kutoka nje ya nchi kutafuta uzoefu zaidi.

Hitimana alianza kuinoa Biashara United ambayo iliamua kumpiga chini kwa kile ilichoeleza kuwa hakuwa na uwezo wa kukinoa kikosi hicho na aliibukia Namungo FC iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo aliipandisha kwa msimu wa 2019/20.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Namungo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 50 kibindoni baada ya kucheza mechi 28.

Kocha huyo amesema: “Muhimu kwa makocha wazawa kutafuta changamoto mpya ili kupata uzoefu kwani maisha lazima yaendelee,”.

SOMA NA HII  MWAKYEMBE AWAONYA WATANZANIA KUHUSIANA NA SAMATTA - VIDEO