Home Uncategorized SERGE NA SISSOKO WA SPURS WAKIUKA SHERIA YA UMBALI

SERGE NA SISSOKO WA SPURS WAKIUKA SHERIA YA UMBALI


NYOTA wa Spurs Serge Aurier na mwenzake Moussa Sissoko wamevunja Sheria ya umbali wa kufanya mazoezi katika kipindi cha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji wengi nchini England na duniani kiujumla wametakiwa kutofanya mazoezi kwa pamoja ikiwa ni kujilinda dhidi ya Corona.

Serge, beki wa kulia wa Spurs alipandisha video akifanya mazoezi na Sissoko bila tahadhari kwenye mitandao ya kijamii kisha akaifuta na ametakiwa kuomba msamaha kwa kukiuka utaratibu wa Serikali.

SOMA NA HII  BAADA YA KAZE KUZINGUA, HAWA HAPA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA