Home Uncategorized BAADA YA KAZE KUZINGUA, HAWA HAPA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA

BAADA YA KAZE KUZINGUA, HAWA HAPA WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA


 KLABU ya Yanga imebadilisha uamuzi wa kuendelea na kocha Cedric Kaze ambaye alitarajiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

 

Kaze awali ilisemekana amemalizana na Yanga amekuwa akiripotiwa kuja nchini kuandaa kikosi cha Yanga kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi inayofikia kilele Agosti 30, 2020 ambapo watacheza na Aigle Noir ya Burundi, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema Kaze ameomba udhuru wa kuchelewa kuja kutokana na matatizo ya kifamilia.


“Kocha Kaze ametuma ujumbe akiomba wiki tatu zaidi kutokana na matatizo hayo, hivyo uongozi umeona ni vyema utafuta kocha mwingine kutoka kwenye orodha ya waliokuwa wameleta maombi awali haraka iwezekanavyo” imeeleza taarifa hiyo.


Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kuingia kwenye hesabu za Yanga ni pamoja na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omong pamoja Kocha Mkuu wa Taifa Stras, Ettiene Ndayiragije.


Kwa sasa Yanga inaendelea na maandalizi kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

SOMA NA HII  KWENYE NGAO YA JAMII AZAM FC INAPATA TAABU KINOMA