Home news MAKOCHA HAWA WAPO KWENYE RADA ZA KAGERA SUGAR, YUPO WA YANGA

MAKOCHA HAWA WAPO KWENYE RADA ZA KAGERA SUGAR, YUPO WA YANGA

 


FRANCIS Baraza Kocha Mkuu wa Biashara United anatajwa kuingia kwenye rada za Kagera Sugar kuziba nafasi ya Mecky Maxime ambaye amefutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu.

Mbali na Baraza pia Ettiene Ndayiragije aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars naye anatajwa kuwa katika rada za mabosi wa Kagera Sugar. 

Pia Ndayiragije alikuwa anahusishwa kujiunga na Yanga kubeba mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifungashiwa virago Machi 7 baada ya ubao kusoma polisi Tanzania 1-1 Yanga.

Jina la Ndayiragije lilikuwa linapewa chapuo kuwa ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kipo mikononi mwa Kaimu Kocha, Juma Mwambusi.

Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud amesema kuwa mchakato wa kumpata Kocha mpya unaendelea.

“Bado mchakato wa kumtafuta kocha mpya unaendelea hivyo mambo yakiwa sawa hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa mashabiki wasiwe na mashaka,”.


SOMA NA HII  MASTAA SIMBA NI GHALI KULIKO WA YANGA....MZAMIRU AWAZIDI THAMANI PACOME NA AUCHO...