Home Yanga SC MRITHI WA KAZE NI MAALUMU KWA AJILI YA CAF

MRITHI WA KAZE NI MAALUMU KWA AJILI YA CAF

 


SEBASTIAN Migne, raja wa Ufaransa anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2020 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na mwendo mzuri.


Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa za Migne kuletwa ni kwa ajili ya mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) ikiwa ni ile ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Imani kubwa ya Yanga ni kwamba wana nafasi ya kushiriki mashindano hayo msimu ujao kwa kuwa wanaamini wapo Kwenye nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara pamoja na lile la Shirikisho. 


Migne aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya na timu ya Taifa ya Equatorial Guinea.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Yanga,Dominic Albinius aliweka wazi kuwa mchakato unaendelea na atakayekuja ni Kocha mwenye uzoefu.

SOMA NA HII  YANGA HAWAJAKATIA TAMAA UBINGWA WA SIMBA