Home Simba SC MSHAMBULIAJI SIMBA AGOMEA OFA YA YANGA MAZIMA

MSHAMBULIAJI SIMBA AGOMEA OFA YA YANGA MAZIMA

 


MUSSA Mgosi, mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Simba ameseka kuwa wakati akicheza soka la ushindani watani wa jadi Yanga walikuwa wakimfuata mara nyingi ili wapate saini yake ila aligoma kwa kuwa alikuwa anaogopa kuonekana msaliti.

Mgosi kwa sasa ametundika daluga akiwa ni Kocha Mkuu wa timu ya Simba Queens inayoshiriki Ligi ya Wanawake Tanzania.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgosi amesema kuwa kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja ilikuwa ni rahisi kwake kupendwa na timu kubwa ila hakuwa tayari kwenda kucheza Yanga kwa kuhofia kuwa msaliti.

“Nilikuwa ninapenda kuwa ndani ya Simba kwa kuwa tulikuwa tunaishi kwa upendo na ushirikiano mkubwa. Kuna wakati mambo yalikuwa magumu ila tulipita kipindi hicho cha mpito hapo nikapata somo kwamba umoja ni nguvu.

“Kweli wakati ninacheza Simba mabosi wa Yanga walikuwa wanahitaji saini yangu, nilikataa kucheza huko haina maana kwamba sio timu nzuri hapana bali niliogopa kuonekana msaliti.

“Maisha yangu ya soka na msingi mkubwa ulijwengwa nikiwa ndani ya Simba hivyo sikuwa tayari kuvunja ule msingi ambao nimetengenezewa kwa muda mrefu,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA MASHABIKI KUMSEMA SANA...BOCCO AVUNJA UKIMA SIMBA...AELEZA KILIO CHA WACHEZAJI WOTE...