Home Simba SC SAKATA LA SIMBA KUPOKWA POINTI TATU NA WASUDAN LIMEFIKIA HAPA

SAKATA LA SIMBA KUPOKWA POINTI TATU NA WASUDAN LIMEFIKIA HAPA


 IMEELEZWA kuwa malalamiko ambayo Klabu ya Al Merrikh ya Sudan wameishtakia Simba yamekwama baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuwaambia kwamba waongeze ushahidi zaidi.

Al Merrikh wlipeleka malalamiko yao mbele ya Caf kwa kueleza kuwa walifanyiwa hujuma na mabosi wa Simba kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochewa Uwanja wa Mkapa.

Kupitia kocha wao mkuu, Lee Clark aliweka wazi kuwa kitendo ambacho walifanyiwa hakikuwa cha kiungwana jambo ambalo liliwafanya wapoteze mchezo wao huo muhimu.

Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mazima ambazo zimewafanya waweze kuongoza kundi A wakiwa a pointi 10, huku Al Merrikh wakiwa na pointi moja ambayo waliipata kwa kulazimisha sare ya bila kufungana na Simba.

Malalamiko ya wapinzani hao wa Simba yalibainisha kuwa walihujumiwa kwa kigezo cha Corona ambapo wachezaji wao 8 waliambiwa kwamba wameathirikia na Corona ikiwa ni muda mfupi kabla ya mechi.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Al Merikh iliweka wazi kwamba wameonewa jambo ambalo wanaamini kwamba ilikuwa ni mbinu ya kuwashinda kiujanja.

Ikiwa malalamiko hayo yatakuwa na tija inaweza kupeekea Simba kupokwa pointi tatu na kupewa adhabu kutokana na sakata hilo jambo ambalo linawapa tabu Al Merikh kupambana ili kupata matokeo haraka.

SOMA NA HII  BAADA YA KUVULIWA UBINGWA JANA...SIMBA 'WAKUBALI KUCHUTAMA'....WAIPIGIA SALUTI YANGA ..WAJIBIWA HIVI...