Home kimataifa CRISTIANO RONALDO BADO YUPOYUPO JUVENTUS NA KOCHA WAKE

CRISTIANO RONALDO BADO YUPOYUPO JUVENTUS NA KOCHA WAKE

 


CRISTIANO Ronaldo ataendelea kubaki kuichezea Juventus hadi mwishoni mwa mkataba wake hiyo ni kwa mujibu wa kigogo wa klabu hiyo.

 

Makamu wa Rais wa Juventus, Pavel Nedved ameyaweka wazi hayo baada ya kuwa na tetesi kuwa Mreno huyo ataondoka mwishoni mwa msimu huu kujiunga na Real Madrid.

 

Ronaldo amekuwa akikosolewa na baadhi ya wachambuzi na mashabiki kwa kutokuwa na msaada kwa timu yake katika michuano ya Ulaya na ile ya Serie A.


“Ana mkataba hadi Juni 30, 2022 na ataendelea kuwa nasi katika kutimiza majukumu yake.


“Kwangu mimi, Cristiano hawezi kuguswa na yeyote katika usajili, ” .


Kiongozi huyo ambaye pia ni kiungo wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Czech, ameongeza kuwa kocha wa timu hiyo, Andrea Pirlo ataendelea kubaki kuongoza kikosi hicho.

 

“Pirlo ataendelea kuwa kocha wa Juventus, huo ni uhakika asilimia 100,” alisema Nedved.


SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WALIKUWA WANAHITAJI SAINI YA KIUNGO WA WATFORD