Home Simba SC SIMBA KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRICAN SUPER LEAGUE

SIMBA KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRICAN SUPER LEAGUE


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kushiriki mashindano ya African Super League ambayo yanatarajiwa kuanza kufanyika hivi karibuni.


Leo Machi 12 nchini Morocco kulikuwa na uchaguzi wa wa CAF nchini Morocco ambapo Rais mpya amepatikana ambaye ni Patrice Motsepe mmiliki wa Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Barbara Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna mpango wa kuanzisha mashindano ya African Super League na yatashirikisha timu 20.

Ikiwa mashindano hayo yataanza kwa Tanzania, Simba itakuwa imepenya jumla kwa kuwa kwa sasa ipo hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Barbara ameandika namna hii kupitia ukurasa wake wa Instagram:”Ulikuwa ni wasaa mzuri kukutana na Rais wa FIFA, Gianni Infantino pembezoni mwa mkutano wa CAF Elections2021. 

“Maandalizi ya kuanza kwa African Super League ambayo itashirikisha vilabu 20 yanaendelea. Tunatarajia kwamba Simba itashiriki hivi karibuni,”.
SOMA NA HII  TETESI:-TRY AGAIN ASUKA MPANGO WA KUMTOA MO DEWJI SIMBA....BAKHRESA ATAJWA KWENYE MIPANGO...