Home Azam FC AZAM FC YAIPIGIA HESABU NAFASI YA YANGA KUKAMILISHA JAMBO LAO

AZAM FC YAIPIGIA HESABU NAFASI YA YANGA KUKAMILISHA JAMBO LAO


 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina umeweka wazi kuwa upo kwenye mpango wa kutumia faida ya matokeo mabaya ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, ili wao wakae juu yao.

 

Mpaka sasa, Azam wapo nyuma ya Yanga kwa tofauti ya pointi sita ambapo Yanga ikiwa imecheza mechi 23 ina pointi 50 na Azam FC ikiwa imecheza mechi 24 ina pointi 44.


 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Tangu mwanzoni mwa msimu huu tuliweka wazi kuwa tuna jambo letu, na hii ni katika kuhakikisha tunajitahidi kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.

 

“Hivyo hatuna presha na mtu aliye nyuma yetu, bali sisi tunamwangalia aliye juu yetu, na kwa sasa Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi, hivyo malengo yetu ni kujitahidi kushinda michezo iliyo mbele yetu ili kupunguza pengo la pointi lililo kati yetu.

 

“Uzuri ni kwamba Yanga nao hawajawa na mwendelezo mzuri na wameangusha pointi nyingi, hivyo ni jukumu letu kulichukulia hilo kama faida na kuwakaribia au hata kuwazidi.”


SOMA NA HII  NYOTA SABA WA AZAM FC WAITWA TIMU YA TAIFA