Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA AUKUBALI MUZIKI WA SIMBA

MBELGIJI WA YANGA AUKUBALI MUZIKI WA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu ya Simba ni miongoni mwa timu kubwa Bongo kutokana na uwezo wake wa kutokata tamaa ya kupambana.

Eymael alikiongoza kikosi chake cha Yanga kuinyoosha Simba kwa bao 1-0 walipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa.

“Simba ni timu kubwa imeweza kuleta ushindani kwenye ligi kwani iliweza kurejea kwenye mstari licha ya kuichapa bao 1-0 tulipokutana kwenye mchezo wetu wa ligi.

“Walifanikiwa kushinda mchezo wao uliofuata mbele ya Singida United kwa ushindi wa mabao mengi (8-0) hii inamaanisha kwamba waliweza kugundua makosa yao na kurejea kwenye ubora,” amesema Eymael.

Yanga baada ya kuitungua Simba kwa bao lililofungwa na Morrison Bernard imecheza mechi mbili na kuambulia pointi moja baada ya kupoteza mechi moja mbele ya KMC na sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo.

SOMA NA HII  TAMBO ZA KOCHA SIMBA BAADA YA KUONDOKA NA ALAMA TATU - VIDEO