Home Simba SC SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MANULA KUPIGIWA HESABU NA TIMU KUBWA ZA AFRIKA

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MANULA KUPIGIWA HESABU NA TIMU KUBWA ZA AFRIKA

 

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa kwa namna kiwango cha kipa wao namba moja Aishi Manula kinavyzodi kuwa bora ipo siku atakuwa ni kipa mkubwa na ataibwa na bara zima la Afrika.

Manula ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amekuwa akitajwa kuwekwa kwenye rada za Klabu ya Al Merrikh ya Sudan ambayo ipo tayari kumuondoa ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leo Machi 28 alianza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon ambapo ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Tanzania 1-0 Libya.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kupitia ukurasa rasmi wa Instagram amesema kuwa uwezo wake uwanjani unamfanya awe sokoni na itafika wakati ataibwa na bara zima la Afrika.

“Hongereni Taifa Stars kwa ushindi. Lakini leo mniruhusu tena nimuongelee Aishi Salum. Huyu kipa kwa sasa yupo katika kiwango bora sana na ndio maana si ajabu klabu kubwa Afrika kumzungumzia. 

“Niliwahi kumwambia mara kadhaa wakati ule Simba au Timu ya Taifa ikifungwa na yeye kuwa wa kulaumiwa, kwamba wewe ni kipa bora mno ila kinachokuponza ni huo muonekano wako tu.

“Kwa sababu makosa yako ni kwa makipa wote duniani. Leo Aishi upo katika top na licha ya kudaka sana pia unafanya saves za hatari iwe kwa Simba au kwa Stars.

“Kwangu mimi Aishi ndio MVP, (mchezaji mwenye thamani) wangu wa msimu huu. Muhimu kamatia hapo hapo, soon, (karibuni) utaimbwa Afrika nzima,” .


SOMA NA HII  SIMBA SC IMEPANIA KURUDISHA UFALME WAKE BAADA YA KUKOSA MATAJI.... LEO KLABU YA SIMBA IMEMTANGAZA MCHEZAJI WAKE HUYU MPYA