Home news INONGA, BANDA NA KAPOMBE WACHUANA TUZO MCHEZAJI BORA SIMBA…SAKHO ACHUNIWA..

INONGA, BANDA NA KAPOMBE WACHUANA TUZO MCHEZAJI BORA SIMBA…SAKHO ACHUNIWA..


Wachezaji watatu Shomari Kapombe, Peter Banda na Henock Inonga wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Februari (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao wamekuwa na takwimu bora zaidi kulinganisha na wengine ambapo mlinda mlango Aishi Manula na nahodha John Bocco walikuwepo katika tano bora.

Katika mwezi Februari Kapombe amecheza mechi nne akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.

Inonga amecheza mechi zote sita za mwezi Februari wakati Banda akicheza nne akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa moja pia.

Zoezi la kupiga kura litaanza leo saa 10 jioni  na kumalizika Jumatano Machi 2, saa 10 jioni.

Mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama zawadi ya kuibuka kidedea.

SOMA NA HII  SHIKILIA HII....KILA BAADA YA DAKIKA TANO....CHOTA PESA KUPITIA CASINO HII YA MERIDIANBET...