Home Habari za michezo KISA MALALAMIKO YA SPORTPESA KWA YANGA…JEMEDARI AIBUKA NA HILI KWA INJINIA HERSI…’AMPOPOA’...

KISA MALALAMIKO YA SPORTPESA KWA YANGA…JEMEDARI AIBUKA NA HILI KWA INJINIA HERSI…’AMPOPOA’ KILA KONA…

Habari za Simba SC

Sakata la Kampuni ya kushashiri ya SportPesa na Klabu ya Yanga limemuibua Mchambuzi wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari, akihoji taratibu zilizochukuliwa na Uongozi wa Klabu hiyo, hadi kufikia hatua ya kukiuka makubaliano na Wadhamini wao.

Yanga juzi Jumatatu (Januari 30) ilisaini mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa Kombe la shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi msimu huu.

Jemedari ametumia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akiandika: “Taarifa hii kutoka SPORTPESA ina kamilisha tu maoni yetu kwamba Yanga SC inaongozwa “KISHIKAJI”. bila kufuata weledi wala utawala bora.

Klabu yenye viongozi imara wenye kufanyakazi kwa kufuata miiko ya uongozi haiwezi kujiingiza kwenye mambo ya KIHUNI kama haya.

Huwa najiulizaga maswali hivi kweli Yanga SC ina idara ya sheria? Kazi yake hasa nini? Mbona kila uchao Yanga wanaingia kwenye mgogoro wa kisheria (kimkataba). Morisson, Feisal, Sportpesa ni mifano tu, yako mengi.

Klabu ishachukua pesa ya SPORTPESA halafu inaenda kuchukua pesa HAIER kwajili ya kitu hicho hicho halafu kwa kuingia mikataba, bado kuna idara ya sheria ya klabu? Huyo mwanasheria kazi yake nini?

Rais wa Yanga SC ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM mpaka leo, Kampuni ya HAIER ni kampuni ambayo ni mshirika mkubwa wa GSM hapa Tanzania, wanapotaka kuitumia Yanga SC kuwekeza Rais wa klabu anasema nini.

Ndiyo maana anashindwa kufuata makataba wa Sportpesa anaamua kuingia wa haier kwakuwa unagusa maslahi yake ya kazini.

Tulikuwa maadui wakati tunatoa maoni ya mgongano wa kimaslahi kumhusu Rais wa klabu tukaitwa majina yote. Lakini hiki ndicho hasa ilikuwa maono yetu. Leo Yanga SC ndiyo hatakama madai itadaiwa klabu, hawa watu wanaweza hata kesho wakaondoka ila klabu itabaki inadaiwa kwa kushindwa kufuata matakwa ya kimkataba.

Bodi ya Wakurugenzi wa Yanga SC walipitishaje hii kitu? Bodi ambayo Makamu wake ni CEO wa Zanzibar Insurance Corporation unaetegemea ajue mambo ya mikataba ya kibiashara akasimama upande wa klabu kwakuwa Rais wake tayari ana maslahi na upande wa pili, lakini naye ni walewale tu, wakute mtandaoni sasa ngebe nyiingi.

SOMA NA HII  WAWAKILISHI WETU KIMATAIFA MNA KAZI YA KUFANYA KIMATAIFA

1 COMMENT

  1. Mimi nadhani huyu Mr Jemedari anadharau sana na hata heshima hana na mimi nadhani cse amewahi kucheza mpira na kipindi hico hali ilikuwa mbaya ki michezo nakumbuka sikosei kusema aliwahi kuvuta bangi .Nasema kwasababu hata kama kuna makosa umeyaona unapochangia jambo ambalo hukulianziasha wewe jaribu kuwa na maoni ya nasikiasiyo kuwa najua huyu bana tha way anavyohandle anything inayoonekana kuwa agaisnt Yanga anakuwa mchochezi na mpondaji upande wa Yanga.Hivi unaposema Yanga inaendeshwa kishkaji wewe mfano hapo Redion ulipo are a qulified Journalist u have a prove na ukimaliza ku prove nitakuuliza maadili ya Uandishi ,hapa sitaki kisingizio cha Uchambuzi.Anavyoongea kama kweli ni mwandishi ni ile isemayo nyani haoni kundule.Nasikia ulinyimwa nafasi ya Afisa habari(alikuhaidi mzee Msola) na na sababu ikiwa ni Elimu na ugomvi na Haji Manara na proof ya hiyo ni mashambulizi na the way you behave towards wrongs the YANGA management unaponda. na swali kweli hii Redio yenu haina watu wa kuzuia taarifa za shutuma kutoka direct.