Home Simba SC SIMBA YATAJA SABABU YA NYOTA WATANO KUBAKI BONGO

SIMBA YATAJA SABABU YA NYOTA WATANO KUBAKI BONGO


UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa za nyota wake watano kuachwa kwenye ardhi ya Tanzania ni mipango ya Kocha Mkuu Didier Gomes mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali.

Jana Machi 3, kikosi cha Simba kilikewea pipa na jumla ya wachezaji  25 kuwafuata wapinzani wao Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi unaotarajiwa kuchezwa Machi 6.

Nyota waliobaki Bongo ni pamoja na mshambuliaji mpya Junior Lokosa, kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, beki wa kati Ibrahim Ame.

Pia yupo kiungo mkabaji Said Ndemla  pamoja na kiungo mshambuliaji Perfect Chikwende ambaye ni ingizo jipya pia kutoka FC Platinum.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa yote ni mipango ya kocha kwa kuwa ameamua kuondoka na wachezaji 25 hivyo hakuna tatizo lolote.

“Mwalimu ameona hawa wachezaji 25 ni sawa hivyo ambao wameachwa kuna sababu ambazo zipo, kwa mfano yupo Chikwende,(Perfect) huyo hata kwenye orodha ya wachezaji wa mechi za kimataifa hayupo.

“Kikubwa ni kuona namna gani kikosi na wachezaji watapambana kwa ajili ya kusaka ushindi ndani ya uwanja,”.

Kwenye kundi A Simba inaongoza kundi ikiwa na pointi sita ina kazi ngumu ya kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh ambayo haijaonja ushindi kwenye mechi zake mbili za Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

SOMA NA HII  LICHA YA KUIBUKA NA GOLI 5 ...HIZI HAPA REKODI ZA KIBABE ZILIZOWEKWA NA SIMBA JANA..