Home Ligi Kuu TIMU ZA BONGO ZATAKIWA KUMUENZI MAGUFULI KWA VITENDO

TIMU ZA BONGO ZATAKIWA KUMUENZI MAGUFULI KWA VITENDO




 KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Beach Soccer, Boniphace Pawasa amesema kuwa ni muhimu kwa timu zote Bongo kuenzi matendo ya Rais John Magufuli kwa vitendo.


Pawasa amesema kuwa kuondoka kwa Magufuli ni pigo kubwa kwa taifa la Tanzania kutokana na kasi yake kwenye kila sekta jambo ambalo linapaswa kuenziwa na timu zote Tanzania.

Pawasa aliongeza pia hata majirani wanatambua namna Magufuli alivyokuwa akiwajibika kwa hali na mali jambo ambalo ni deni kwa timu za Tanzania.

“Timu zote Tanzania ukianza na Simba pamoja na Namungo ambazo zinawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa ni lazima zifanye kazi kwa vitendo kuenzi mchango wa Magufuli.

“Hakuna kingine ambacho Azam FC, Ihefu, Yanga, Kagera Sugar na timu zote Tanzania zinatakiwa kukifanya kwa kuyakumbuka yale mazuri ya Magufuli kwa kufanya mazuri kwenye kazi zao pamoja na mashindano ambayo watashiriki,” amesema.

SOMA NA HII  KATWILA: NIMEWAAMBIA WACHEZAJI KWAMBA KUNA KAZI YA KUFANYA