Home epl TOTTENHAM YACHAPWA NA ARSENAL, LAMELA APIGA BONGE MOJA YA BAO

TOTTENHAM YACHAPWA NA ARSENAL, LAMELA APIGA BONGE MOJA YA BAO

 


LICHA ya Eric Lamela nyota wa kikosi cha Tottenham Hotspur kupachika bao kali mtindo wa rabona mapema dakika ya 33 kwenye London Dabi,  walikwama kusepa na pointi tatu mbele ya Arsenal,  Uwanja wa Emirates. 

Lamela ambaye aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Son-Heung min ambaye aliumia hakutumia muda mrefu kupachika bao hilo.

Alipokea pasi ya Lucas Moura ambaye alimtengenezea pasi hiyo kisha Lamela akapitisha kwenye miguu ya Thomas Partey kisha ukapenya ndani ya nyavu na kufanya liwe moja ya bao bora ndani ya Ligi Kuu England.

Bao la Lamela lilidumu dakika 11 kwa kuwa liliwekwa sawa na Martin Odegaard dakika ya 44 na kuwafanya waende mapumziko ubao ukisoma Arsenal 1-1 Tottenham Hotspur. 


Alexandre Lacazette alipachika bao la ushindi kwa Arsenal kwa mkwaju wa penalti dakika ya 64 na kuwafanya wasepe na pointi tatu mazima huku Lamela akionyesha kadi nyekundu dakika ya 76.


Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 41 ikiwa nafasi ya 10 ma Tottenham inabaki na pointi 45 ikiwa nafasi ya 7.

SOMA NA HII  KOCHA WA REAL MADRID ZIDANE KUTIMKA MAZIMA