Home Yanga SC YANGA WAMVUTIA KASI DAVID MOLINGA

YANGA WAMVUTIA KASI DAVID MOLINGA


 INAELEZWA kuwa, uongozi wa Yanga upo kwenye hesabu za kumrejesha kundini mshambuliaji wao wa zamani David Molinga ‘Falcao’ kwa lengo la kutaka kumrudisha msimu ujao.

Yanga waliachana na mshambuliaji huyo msimu uliopita akiwa amefunga mabao 12 ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo msimu huu mpaka sasa timu hiyo ikicheza mechi 23, hakuna mchezaji wa timu hiyo aliyefikia idadi hiyo.


Kwa sasa kinara wa mabao ndani ya Yanga katika Ligi Kuu Bara ni Deus Kaseke mwenye sita. Michael Sarpong na Yacouba Songne wametupia mabao mannemanne.


Molinga kwa sasa yupo ndani ya Klabu za Zesco United ya nchini Zambia. Inatajwa kuwa yupo kwenye rada za Yanga ili kurejea kuongeza makali. 

 

SOMA NA HII  DIARA AZIDI KUIPAISHA JUU LIGI YA TANZANIA...AITWA TENA MALI KWA KOMBE LA DUNIA...