Home epl CARRAGHER ANA MASHAKA KUHUSU LIVERPOOL KUWA NDANI YA NNE BORA

CARRAGHER ANA MASHAKA KUHUSU LIVERPOOL KUWA NDANI YA NNE BORA


BINGWA wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jamie Carrager amesema kuwa kikosi cha Liverpool kinachonolewa na Jurgen Klopp hakitamaliza ndani ya nafasi nne za juu msimu huu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu England.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England wamekuwa kwenye mwendo wa kusuasa msimu huu jambo ambalo linatokana na wachezaji wake wengi muhimu kusumbuliwa na majeraha.

Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi hicho cha Liverpool amesema kuwa bado anaona kuna gepu kubwa ambalo timu hiyo imeachwa jambo litakalowafanya washindwe kumaliza wakiwa ndani ya nafasi nne za juu.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 29 ipo nafasi ya 6 na pointi zake ni 46, imeachwa kwa tofauti ya pointi 25 na vinara ambao ni Manchester City wakiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 30. 

Carrager amesema:”Bado kuna gepu kubwa ipo ila kwa sasa siamini kama Liverpool itaingia kwenye nne bora,” .

SOMA NA HII  ISHU YA MECHI KUAHIRISHWA, MESSI AMECHUKIA KWELIKWELI