LICHA ya makosa ambayo amekuwa akiyafanya ya mara kwa mara ndani ya uwanja, beki wa kati wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, ni jembe la kazi kwa kuwa kila mechi atakayoanza amekuwa akiyeyusha dakika zote 90.
Miongoni mwa makosa ambayo aliyafanya Mwamnyeto yakasababisha timu yake kufungwa ni pamoja na pasi aliyotoa kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa iliyosababisha bao wakati ubao ukisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting.
Pia alirudia kosa hilo wakati ubao ukisoma Yanga 3-3 Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa jambo ambalo lilikuwa likiigharimu timu hiyo inayoongoza ligi na pointi 50.
Akiwa ni ingizo hilo jipya msimu huu akitokea Coastal Union, amecheza mechi 20 kati ya 23 ambazo Yanga imecheza na kutumia jumla ya dakika 1800.
Mechi alizocheza ni dhidi ya Prisons, Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Polisi Tanzania, KMC, Biashara United na Simba.
Zingine ni Namungo, Azam, JKT Tanzania, Ruvu Shooting, Mwadui, Dodoma, Ihefu, Prisons, Mbeya City, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar.
Kwenye mechi hizo zote beki huyo alimaliza dakika zote 90.