KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola inaelezwa kuwa amependekeza jina la mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haalad kusajiliwa katika kikosi hicho msimu ujao.
Haalad amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Manchester United, Chelsea pia hata Real Madrid inayoshiriki La Liga nayo imekuwa ikitajwa.
City kwa sasa ipo mawindoni kumsaka mbadala wa mshambuliaji wao Sergio Arguero ambaye msimu ukimeguka anasepa kwenye kikosi hicho kwa kuwa taarifa rasmi kutoka ndani ya kikosi hicho zimeeleza kwamba hataongeza mkataba.
Dau ambalo wameweka mezani ili kumpata nyota huyo inaelezwa kuwa ni Euro milioni 100 licha ya Guardiola kuweka wazi kwamba wamekubaliana kutotumia dau kubwa kwa ajili ya mchezaji mmoja.
“Klabu imekubaliana kutotumia zaidi ya Euro milioni 100 kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji mmoja, labda kwa wakati ujao ambapo inaweza kukubalika. Na itakuwa kwa ajili ya maelngo ya miaka 10 ama mitano mbele.
“Kutumia fedha nyingi kwa ajili ya mchezaji mmoja naona kwangu sio sawa kwa sababu hupati ushindi kupitia mchezaji mmoja bali timu kiujumla kwa namna inavyocheza. Mpira ni ushikrikiano kwa sababu kwenye mashindano kwa kila mmoja ambaye anafanya hivyo inakuwa rahisi kupata matokeo,” amesema.
Haalad ametupia jumla ya mabao 33 akicheza jumla ya mechi 32 kwa msimu huu akiwa na umri wa miaka 20.