Home Simba SC GOMES AWAANDALIA “SAPRAIZI” WAARABU KESHO

GOMES AWAANDALIA “SAPRAIZI” WAARABU KESHO


KIKOSI cha Simba leo kitaendelea kujifua kwa mara ya mwisho kuanzia saa 3:00 usiku kabla ya mchezo wao wa kesho Ijumaa dhidi ya Al Ahly, huku Kocha Mkuu Didier Gomes akijiandaa kuwasapraizi wenyeji wao, waliouhamisha mchezo huo kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Cairo hadi ule wanaoumiliki wao wa Al Salaam WE.

Simba itajifua kwenye uwanja huo kwa mchezo wao wa kesho Ijumaa utakaopigwa kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (sawa na saa 3:00 usiku wa Cairo) ili kuhitimisha mechi za Kundi A za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kulingana na mazoezi ya Simba ambayo yalifanyika jana Jumatano muda kama ambao yatafanyika mazoezi ya leo kunaweza kuwa na mabadiliko katika maeneo mawili tofauti.

Gomes amepanga kuisapraizi Al Ahly kwa kuingia na kikosi tofauti na kile kilichocheza mechi yao ya jijini Dar es Salaam na Waarabu hao kulala 1-0 na pia tofauti na kikosi kilichocheza na As Vita ya DR Congo na kuwafumua mabao 4-1.

Kulingana na kikosi cha Simba ambacho kimekuwa kikianza mara kwa mara au kile ambacho kilicheza mechi ya mwisho hapa Dar es Salaam, mabadiliko hayo yanaweza kufanyika katika eneo la kiungo pamoja na ushambuliaji.

Gomes amesema mchezo wa kesho ni mgumu, lakini ataangalia namna wachezaji wake watakavyofanya mazoezi ya mwisho, lakini akisisitiza kutakuwa na mabadiliko katika baadhi ya wachezaji.

Kwa taarifa zaidi ya mabadiliko ya wachezaji ambao huenda kesho hawatacheza pambano hilo usikose kusoma ndani ya Gazeti la Mwanaspoti la kesho Ijumaa na mitandao yetu ya kijamii.

SOMA NA HII  GAMONDI ATUMIA DAKIKA 180 KUWASOMA SIMBA