Simba SC

CHAMA AWEKA REKODI YA PASI ZA MWISHO BONGO

admin April 15, 2021 3:47 pm

 NYOTA wa Simba Clatous Chama ameweka rekodi ya kuwa namba moja kwa wanaotengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar,  Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikifikisha jumla ya pointi 49 Chama amefikisha pasi 10.

Mbali na kuwa na pasi 10 pia nyota huyo ametupia jumla ya mabao 7 kwa msimu huu akiwa ni moja ya viungo bora wanaofanya vizuri ndani ya ligi.

Anayemfuata kwa kuwa na pasi nyingi za mwisho ni Luis Miquissone ambaye naye anacheza  Simba akiwa na pasi 9 za mabao.

David Luhende wa Kagera Sugar beki mzawa ambaye ana pasi nyingi za mabao akiwa nazo 7 pia ana bao moja.

YANGA: TUTAJIULIZA WAPI AMBAPO TUMEKUWA TUKIKOSEA KWA BIASHARA UNITED VIDEO: YANGA WATOA TAMKO KUHUSU MANJI KURUDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply