Simba SC

KAGERE: NINAPENDA KUFUNGA KWA KUWA NI KAZI YANGU

admin April 16, 2021 12:47 pm

 


MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anapenda kufunga muda mwingi akiwa uwanjani jambo linalomfanya aongeze juhudi.

Ndani ya Ligi Kuu Bara,  Kagere ametupia jumla ya mabao 11 na timu yake imekusanya jumla ya pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. 

Namba moja ni watani zao wa jadi Yanga ambao wamekusanya pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.

Kagere amesema:”Ninapenda kufunga kwa kuwa mimi ni mshambuliaji na kila mshambuliaji anapenda kufanya hivyo kila akianza.

“Ushindani ni mkubwa nasi pia tunapambana ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu,”.

Msimu uliopita Kagere alitupia mabao 22 na alisepa na kiatu cha ufungaji bora.

MCHORA RAMANI WA SIMBA HESABU ZAKE NI MECHI ZA CAF KIKOSI CHA KMC LEO DHIDI YA GWAMBINA FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply