Simba SC

ISHU YA UWEKEZAJI SIMBA YAJA KIVINGINE, SERIKALI YATOA TAMKO

admin April 18, 2021 9:47 pm

 


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amebainisha kwamba, leo Jumatatu, Simba na Tume ya Ushindani (FCC) watakutana ili kujadili hatima ya suala la uwekezaji ndani ya klabu hiyo.


Hayo yametokea mara baada ya waziri huyo kujibu swali bungeni aliloulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Tanga, Rashid Abdallah Shangazi alipoulizwa juu ya suala la uwekezaji ndani ya Simba.

 

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kuonesha kuilalamikia FCC kuchelesha suala la mabadiliko ndani ya Simba.


Waziri Bashungwa alisema kuwa, Serikali imelitazama jambo la FCC na uwekezaji wa Simba, hivyo watafanya kila liwezekanalo ili jambo hilo kukamilika kwa haraka zaidi ili Simba waingie katika mfumo mzuri wa mabadiliko ya kiuendeshaji.


“Serikali tumelitizama jambo hili na tutalifanyia kazi ili Simba waweze kufanikisha jambo hili, hivyo Jumatatu Simba watakaa kikao na FCC ili kuendelea kuangalia watafanikisha vipi jambo hili la uwekezaji ndani ya Simba,” alisema Waziri Bashungwa.

MANCHESTER UNITED YATEMBEZA 3G MBELE YA BURNLEY VIDEO: YANGA YAZUNGUMZIA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA BIASHARA UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply