Simba SC

SIMBA YATAMBIA NA REKODI YAO CAF, HESABU ZAO ZIMECHORWA NAMNA HII

admin April 19, 2021 10:47 am


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier 
Gomes, amesema kwamba, msimu huu anataka kurudia mafanikio yake ya kufika nusu fainali kwenye michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kocha huyo raia wa Ufaransa, ameongeza kwamba, anataka kurudia rekodi hiyo ya mafanikio makubwa ambayo aliiweka akiwa anainoa Cotton Sports ya Cameroon walipofika nusu fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu huu, Gomes ameiongoza Simba kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakimaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi A kwa kukusanya pointi 13.

Kocha huyo mwaka 2014 aliifanikisha Cotton Sports kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo walitolewa na Al Ahly.

“Tulicheza nusu fainali nikiwa na Cotton Sports kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya Al Alhy, lakini tukapoteza, nina matumaini makubwa ya kufika mbali na kikosi ambacho ninacho kwa sasa.

“Bado kazi inaendelea, tunatakiwa kupambana zaidi kuliko ilivyokuwa miezi mitatu iliyopita na kikubwa tunatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa sababu michezo inayokuja ni hatari sana,” aliweka nukta kocha.


BREAKING: JOSE MOURINHO AFUTWA KAZI SPURS KUMEKUCHA YANGA, KOCHA HUYU KUPEWA MIKOBA YA KAZE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply