KUELEKEAkwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, uongozi wa Gwambina FC umewatengea mkwanja wachezaji wake ili waifunge Simba leo.Timu hizo zinatarajia kumenyana leo kwenye Uwanja wa Gwambina Complex uliopo Misungwi, Mwanza, ambapo kwenye mchezo wa kwanza Gwambina ilikubali kichapo cha mabao 3-0.
Mabao hayo zama za Sven Vandenbroeck wa Simba,yalifungwa na Meddie Kagere, Pascal Wawa na Chris Mugalu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Gwambina, Mohamed Badru alisema kuwa: “Wachezaji wote wapo fiti kuelekea kwenye mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Simba.“
Tunafahamu kuwa tunaenda kukutana na timu kubwa yenye ushindani lakini tutapambana ili kuhakikisha tunapata ushindi kwenye uwanja wetu wa nyumbani.“
Kwenye michezo miwili iliyopita tumepoteza lakini kadri timu inavyocheza kila siku naona kuna maendeleo makubwa na makosa yanapungua.
“Kuna kiasi cha bonasi kwa wachezaji kimewekwa na uongozi kwa ajili ya kuongeza morali ya wachezaji kupambana ili timu ibaki ligi kuu.”Gwambina inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi 30 ikiwa imecheza mechi 25.
STORI: LEEN ESSAU, CHAMPIONI JUMAMOSI