Home news WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA

WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA


WAZIRI wa Maliasili  na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.


Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma  kuanzia 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni.

Ametoa agizo  hilo wakati  akizindua msimu wa saba wa Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji  ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai  kwa muda wa siku saba mkoani hapo.



Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo ” Misitu ni Uchumi ” Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa  Jamii  kutunza misitu zaidi.


 Ndumbaro amesema anategemea tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali  kuanza kutembelea  vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba Lipalamba.

Katika hatua nyingine, amemuomba mkuu wa  wilaya ya Songea  kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake kushiriki katika tamasha hilo.

” Mkuu wa wilaya najua una taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki tamasha la Majimaji Selebuka ” alisisitiza Ndumbaro. 


Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki tamasha hilo na   ametumia fursa hiyo kuziomba taasisi nyingine za watu binafsi kushiriki katika tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa tamasha hilo.


Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, Wanamichezo, Wanafunzi, na Wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini. 



SOMA NA HII  MASTAA AZAM FC WAFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA YANGA SC...MMOJA ACHOMOA...