Simba SC

ZIMBWE Jr AFUNGUKA UGUMU WA MECHI DHIDI YA GWAMBINA

admin April 25, 2021 10:52 am

 


Mfungaji wa bao pekee katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Gwambina FC, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mazingira ya Uwanja wa Gwambina hayakuwa rafiki jambo lililosababisha mechi kuwa ngumu.

Zimbwe amesema iliwalazimu wachezaji kucheza soka la mipira mirefu ya juu sababu uwanja haukuruhusu soka letu la kawaida la pasi fupi fupi tulilolizoea.

Mlinzi huyo wa kushoto amesema amefurahi kufunga bao la ushindi ambalo limetuwezesha kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu huu ulipoanza.

“Tulisubiri kwa muda mrefu siku hii kufika na tulipambana hadi kufanikisha kukaa kileleni, binafsi nimefurahi kufunga bao la ushindi ambalo limetupandisha hadi nafasi ya kwanza,” amesema Zimbwe.

Zimbwe ameongeza kuwa malengo ya timu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kutetea ubingwa ambapo kama tutafanikiwa itakuwa ni mara ya nne mfululizo.

WAZIRI NDUMBARO AZITAKA WIZARA KUSHIRIKI MAJIMAJI SELEBUKA YANGA V AZAM FC KWA MKAPA LEO KITAUMANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply