NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa atapambana ili kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha mpya wa Yanga, Nasreddine Nabi.
Niyonzima kabla ya kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze alikuwa akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Baada ya timu kukabidhiwa kwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi bado nafasi yake imekuwa ngumu ambapo kocha huyo amekuwa akimwamini zaidi Carlos Carlinhos.
Akizungumza na Championi Jumatano Niyonzima alisema kuwa: “Kikosi cha Yanga kipo vizuri kwa sasa na matarajio ya kutwaa ubingwa yapo, sisi hatumwangalii mpinzani wetu ila kwa sasa tunadili na michezo yetu iliyobaki ya ligi na kupata pointi tatu ili kutimiza malengo yetu.
“Najiamini na ninajikubali hivyo nitajituma mazoezini kwa ajili ya kuhakikisha ninakuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi chake ila siwezi kusema nina uhakika huo kwa sasa,” .