Home Azam FC KIPA NAMBA MOJA WA AZAM FC KUIBUKIA JKT TANZANIA

KIPA NAMBA MOJA WA AZAM FC KUIBUKIA JKT TANZANIA


KIPA namba moja wa Klabu ya Azam FC kwa sasa Mathias Kigonya anaendelea vizuri mara baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kuna asilimia kubwa kwamba kipa huyo huenda akaibuka kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania ikiwa hali yake itatengamaa.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Aprili 9, ubao ulisoma Azam FC 2-0 Mtibwa Sugar na mabao yote yalifungwa na Prince Dube ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 10.

Kigonya hakumaliza dakika 90 kwa kuwa alipata maumivu ya bega. Taarifa kutoka Azam FC zimeeleza kuwa nyota huyo anaendelea vizuri.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa baada ya kupata maumivu alikuwa chini ya jopo la madaktari ambao walikuwa wanamshughulikia hali yake.

“Kila kitu kinakwenda sawa na Kigonya hali yake kwa sasa ni nzuri kwani anaendelea na matibabu huenda anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza dhidi ya JKT Tanzania, Aprili 16,” .

Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya pili na ina pointi 47 baada ya kucheza jumla ya mechi 25 inakutana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 12 na pointi 27.

SOMA NA HII  DILI LA KAHATA KUIBUKIA AZAM FC LIMEKUWA GUMU