Home Simba SC MKATA UMEME LWANGA KUWAKOSA DODOMA JIJI LEO KWA MKAPA

MKATA UMEME LWANGA KUWAKOSA DODOMA JIJI LEO KWA MKAPA


 KIUNGO Mkabaji wa Klabu ya Simba, Taddeo Lwanga ataukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes saa 1:00 itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata ambapo itakosa huduma ya mkata umeme huyo.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa watamkosa Lwanga kwa kuwa alipata msiba wa dadayake.

“Tutakosa huduma ya Taddeo Lwanga kwa sababu ana msiba wa dada yake hivyo tunamuombea Mungu ampe nguvu ili aweze kumaliza mambo hayo kisha ajiunge na timu.

“Kuhusu maandalizi kila kitu kipo sawa na tunahitaji kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,”.

Aprili 23, Simba walitoa salamu za rambirambi kwa mchezaji huyo kwa kumpa pole juu ya kuondokewa na dada yake mpendwa Agnes Nakityo.

Kutokana na msiba huo Lwanga alikosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC uliochezwa Aprili 24 Uwanja wa Gwambina Complex na ubao ulisoma Gwambina 0-1 Simba, ilikuwa ni siku ya mazishi kwenye kijiji cha Ndejje Kanyanya Zone kilichopo mjini Wakiso, Uganda.


 

SOMA NA HII  BREAKING: MUGALU MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA