Home Ligi Kuu KMC WAFUNGUKIA KUHUSU UBINGWA WA LIGI KUU BARA

KMC WAFUNGUKIA KUHUSU UBINGWA WA LIGI KUU BARA


 KOCHA Msaidizi wa KMC, Habib Kondo amesema kuwa kwa sasa hawana hesabu za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Simba na badala yake hesabu zao ni kushinda mechi zao zilizobaki.


Kwa sasa kuna vita kubwa ya ubingwa ambapo timu tatu zinapewa nafasi ya kuweza kusepa nao ikiwa ni pamoja na vinara Yanga, mabingwa watetezi Simba pamoja na Azam FC.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kondo alisema kuwa kwa sasa hawafikirii kutwaa ubingwa wa ligi badala yake watapambana kuweza kupata ushindi kwenye mechi zao.

“Hatuhitaji kutwaa ubingwa wa ligi kwa sasa huo tunawaachia Yanga na Simba hao acha wapambane huko ila sisi malengo yetu ni kumaliza kwenye tano bora na inawezekana hata wachezaji wanajua,” alisema Kondo.

KMC kwenye msimamo ipo nafasi ya tano ina pointi 40 baada ya kucheza mechi 27.

SOMA NA HII  TANZANIA PRISONS MGUU SAWA KUENDELEA NA PIRA GWARIDE