Home Ligi Kuu TANZANIA PRISONS MGUU SAWA KUENDELEA NA PIRA GWARIDE

TANZANIA PRISONS MGUU SAWA KUENDELEA NA PIRA GWARIDE


 SHABAN Kazumba, kocha msaidizi wa kikosi cha Tanzania Prisons amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Tanzania Prisons ipo nafasi ya 8 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 kwa msimu wa 2020/21.

Imeshinda mechi 7, sare 10 na imepoteza jumla ya mechi 6 na ina pointi zake kibindoni 31.

Mechi yao ya ufunguzi msimu huu ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa na iliporudiana nao mara ya pili, Uwanja wa Nelson Mandela, ubao ulisoma Prisons 1-1 Yanga.

Kazumba amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu za ligi na tunaamini kwamba tutapata matokeo chanya hivyo kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki.

“Wachezaji wapo imara na kila mmoja ana morali kubwa ya kusaka ushindi na tunahitaji kumaliza ligi tukiwa kwenye nafasi nzuri,” .

Mchezo wake ujao wa ligi ni dhidi ya Dodoma Jiji, unatarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Nelson Mandela.

SOMA NA HII  YANGA KUIFUATA JKT TANZANIA KWA TAHADHARI LEO