Home Ligi Kuu KMC YATUMA SALAMU KWA BIASHARA UNITED

KMC YATUMA SALAMU KWA BIASHARA UNITED

 KMC FC kesho kazini tena

Mara baada ya kuibuka na ushindi wa maba 3-0 dhidi ya Gwambina, kikosi cha KMC kesho kitakuwa katika mchezo mwingine dhidi ya Biashara utakaopigwa saa 8:00 mchana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

KMC FC watakuwa ni wenyeji katika mchezo huo dhidi ya Biashara inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 ikiwa ugenini katika uwanja wa CCM Karume Musoma Mkoani Mara timu hizo mbili zilipokutana katika duru ya kwanza.

Aidha katika mchezo  kesho KMC FC inahitaji ushindi iliiweze kuendelea kujiimarisha zaidi katika nafasi za msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania na hivyo kufikia malego ambayo kama timu ilijiwekea nia ya kumaliza ligi ikiwa kwenye nafasi nzuri.

Licha ya kwamba katika mchezo huo kutakuwa na upinzani mkubwa  kikosi kilichopo kutokana na maelekezo ambayo wamepewa na Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa wachezaji hao wanaamini watashinda.

KMC FC inahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili kuiwezesha timu kupanda katika nafasi  Nne za juu ambayo kwa hivi sasa inashikiliwa na Timu ya Biashara.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema:-“ Tunakwenda kwenye mchezo ambao kimsingi tunafahamu kabisa utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu ambayo tunakutana nayo, wanafanya vizuri, lakini pia wako kwenye nafasi ya nne hivyo tumejipanga kuingia kwenye mchezo huo pasikuwa na  hofu,” .

Hadi sasa Timu ya KMC ipo katika nafasi ya tano na kwamba katika mchezo uliopita dhidi ya gwambina, iliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri, ambayo  yalifungwa na Charles Ilamfya, Ally Ramadhani pamoja na Emmanuel Mvuyekule.

SOMA NA HII  MBEYA KWANZA WATAJA SABABU YA KUPANDA LIGI KUU BARA