Home Ligi Kuu MBEYA KWANZA WATAJA SABABU YA KUPANDA LIGI KUU BARA

MBEYA KWANZA WATAJA SABABU YA KUPANDA LIGI KUU BARA


STEVEN Matata, Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza amesema kuwa ushirikiano ambao alikuwa anapata kutoka kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi ndani ya Ligi Daraja la Kwanza ni sababu kubwa iliyoifanya timu hiyo kupanda daraja.

Timu hiyo ambayo ipo kundi A ndani ya Ligi Daraja la Kwanza ilitimiza malengo yake ya kupanda Ligi Kuu Bara, Aprili 25 kwa kupata ushindi dhidi ya African Sports wa bao 1-0.

Matata amesema kuwa ni furaha kwa timu kiujumla kuweza kufanikiwa kupanda kwenye ligi kwa kuwa ilikuwa ni mipango iliyokuwa inapewa kipaumbele.

“Ninawapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na uongozi wa timu kwa kunipa ushirikiano, ushirikiano ambao tulikuwa tunapeana umesababisha tumeweza kufanikiwa malengo yetu ya kupanda ligi.

Mbeya Kwanza imecheza jumla ya mechi 15 imekusanya pointi 38 ipo nafasi ya kwanza huku African Sports ikiwa nafasi ya pili na ina pointi 28. Kwa msimu wa 2021/22 itakuwa ndani ya Ligi Kuu Bara huku ikisubiria kuona ni timu zipi ambazo zitashuka kutoka kwenye  Ligi Kuu Bara mpaka Ligi Daraja la Kwanza.


SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA, SIMBA YAISHUSHA YANGA