Home Habari za michezo KONDO AIPELEKA SIMBA NUSU FAINAL SHIRIKISHO AFRIKA…AWAMALIZA WASAUZI NNJE YA UWANJA…

KONDO AIPELEKA SIMBA NUSU FAINAL SHIRIKISHO AFRIKA…AWAMALIZA WASAUZI NNJE YA UWANJA…


Aliyekuwa kocha msaidizi wa KMC, Habib Kondo ameipigia chapuo Simba SC kuibuka na ushindi dhidi ya Orlando Pirates, kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho uliopangwa kuchezwa Aprili 17 na ule wa marudio tarehe 24 mwezi huu.

Kondo anasema hayo kutokana na ubora wa Simba waliofuzu hatua robo fainali mara tatu katika miaka mitano, wakifuzu mara mbili kwenye ligi ya mabingwa 2018/2019, 2020/2021 na mwaka huu kwenye kombe la shirikisho.

”Orlando ni timu ya kawaida tu kwa Simba, kwasababu Simba ni Bingwa wa Tanzania, na ni mwamba wa Afrika hivi sasa ameshazifunga timu kubwa zaidi ya Orlando, washazifunga Al Ahly, Zamaleki, hivyo huwezi kusema Simba watatishiwa na Orlando, cha msingi ni kujiandaa kucheza kama walivyocheza mechi nyingine ili wapate matokeo”

”Cha msingi Simba wajue kuna mechi moja itakuwa ni yao waicheze kwa upande wao na kutakuwa na mechi ngingine itakuwa ni ya Orlando Pirates ambayo watakuwa kwao, ni vyema tahadhali ikachukuliwa wapate matokeo ya nyumbani kwakuwa na wapinzani wao watakuwa wanawekeza zaidi kwenye mechi yao ya marudiano” alisema Kondo .

Simba walifuzu hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na alama 10 sawa na vinara RS Berkane waliokuwa na mabao mengi ya kufunga (11)

SOMA NA HII  SAA CHACHE BAADA YA 'KUTUMBULIWA' AZAM FC...LWANDAMINA AANIKA HILI ..'AUVAMIA' UONGOZI...