Home Yanga SC KOCHA MWAMBUSI ATAJA SABABU ZA KUTOFAUTIANA NA KAZE YANGA

KOCHA MWAMBUSI ATAJA SABABU ZA KUTOFAUTIANA NA KAZE YANGA


KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma 
Mwambusi, ametetea uamuzi wake wa kumpanga mshambuliaji, Yacouba Sogne kama mshambuliaji wa kati, tofauti na alivyokuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni chini ya kocha Cedric Kaze, kwa kusema nyota huyo anakuwa hatari zaidi akicheza katikati.


Yacouba amefunga mabao mawili chini ya Mwambusi akiwa kwenye nafasi hiyo ambapo alifunga kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na alifunga kwenye ushindi  wa bao 1-0 katika mchezo wao dhidi ya Biashara United baada ya kufunga bao pekee katika mchezo huo, huku bao hilo

Raia huyo wa Burkina Faso ambaye chini ya aliyekuwa kocha wa Yanga, Kaze alikuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji kwa kutokea pembeni, sasa amefanikiwa kuhusika katika mabao 10 ya Yanga akifunga mabao sita na kutoa asisti nne katika michuano ya Ligi Kuu Bara.


Mwambusi amesema: “Ni kweli chini ya aliyekuwa kocha wetu mkuu Cedric Kaze Yacouba alicheza kutokea pembeni mara nyingi, lakini kwa upande wangu baada ya kuchukua timu kama kocha mkuu nimeamua kumbadilishia majukumu na kuamua kumpanga katika eneo la katikati.

“Hii ni kwa sababu najua Yacouba ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kutengeneza nafasi, anaweza asifunge yeye lakini ana uwezo mkubwa wa kutengenezea nafasi kwa wengine kufunga, na hili limeonekana katika michezo miwili iliyopita ambayo amefanikiwa kufunga mabao mawili.”

Kwenye msimamo wa ligi Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 57, tayari imeshamleta mbadala wa Kaze ambaye ni Nasreddine Nabi ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu.


SOMA NA HII  SIMBA, YANGA KABLA YA LIGI KUANZA KIMESHAUMANA MAPEMAAA