Home kimataifa MANCHESTER UNITED YAISHUSHIA KICHAPO ROMA EUROPA LEAGUE

MANCHESTER UNITED YAISHUSHIA KICHAPO ROMA EUROPA LEAGUE


USHINDI wa mabao 6-2 ambao wameupata Manchester United mbele ya Roma kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza mbele ya Roma unawapa nafasi ya kuweza kutinga fainali.


United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksajer iliweza kufanya vizuri usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa Europa League uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.


Ni Bruno Fernandes dk 9 na dk 71 alitupia kwa penalti,  Edinson Cavani dakika ya 48 na 64 Paul Pogba dakika ya 75, Mason Greenwood dakika ya 86 hawa walifunga mabao ya United kwa Roma ni Lorenzo Pellegrini dakika ya 15 kwa penalti na Edin Dzeko dakika ya 33.

Ole amesema kuwa amefurahishwa na uwezo wa wachezaji wake kwa kuwa walitumia uzoefu wao kusaka ushindi kwenye timu kubwa na mchezo ambao ulikuwa na ushindani muda wote.
SOMA NA HII  LICHA YA KUPOTEZA, MOURINHO ASISITIZA ANAONA MOYO WA UPAMBANAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here