Home Simba SC MANULA : – TUNATATAKA KUWEKA REKODI NGUMU KUFUTIKA CAF

MANULA : – TUNATATAKA KUWEKA REKODI NGUMU KUFUTIKA CAF


KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema wanataka kuandika rekodi ambayo itakuwa ngumu kufutika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf).

Simba leo saa 10 jioni itakuwa wenyeji wa AS Vita ya DR Congo kwenyer Uwanja wa Benjamin Mkapa na Manula alisema licha ya kuifunga kwao wanatambua ni timu ngumu yenye wachezaji wapambanaji, hivyo wanajifua ili kujiwekea misingi imara ya kuweka rekodi ya aina yake.

“Binafsi nina ‘klinishiti’ nne na natamani kuweka nyingine zaidi, ingawa katika yote hayo tunatanguliza maslahi ya timu kuhakikisha inaiwakilisha nchi vyema, lakini tunatambua ni mchezo mgumu ndio maana tumejipanga vilivyo ili kushinda,” alisema Manula.

Aidha Manula alisema ubora alionao katika kikosi hicho cha Simba wakati huu unatokekana na kuwahi kufanya kucheza kwa pamoja na makipa wenzake wazoefu ambao walimtangulia katika nafasi hiyo.

Manula alisema hapa Simba aliwahi kufanya kazi na Said Mohammed ‘Nduda’ ambaye tangu akiwa mdogo aliwahi kumuona na kuvutiwa naye akiwa anacheza baada ya kuja kwao Morogoro wakati huu bado hata hajaanza kufahamika.

Alisema misimu miwili iliyopita hapa Simba amewahi kucheza na Deo Munishi ‘Dida’ ambaye ni moja ya makipa wenye uwezo na uzoefu kwa vile amewahi kucheza timu tatu kubwa za hapa nchini, amecheza nje ya nchi na Taifa Stars.

“Wakati nacheza hapa Simba nikiwa pamoja na makipa hao wawili wazoefu kuna mambo mengi ambayo nilikuwa najifunza kutokea kwao na nilikuwa navifanyia kazi vya kutosha pengine ndio maana nami wakati huu naonekana nacheza katika kiwango kizuri,” alisema.

“Bado sijaacha kujifunza hata wakati huu kutoka kwa makipa wazoefu lakini pia muda mwingi huwa napenda kusikiliza maagizo ya makocha wangu vile ambavyo wanataka nikafanye uwanjani na ndio huwa inatokea hivyo pengine ndio maana wakati huu naonekana kuwa bora.

“Bado nipo na kazi kubwa ya kufanya mbele yangu kwanza kulinda uwezo ambao unaonekana sasa hivi kutoka kwangu lakini pi kujiboresha na kufanya zaidi ikiwemo kuisadia timu kufikia mafanikio lakini kuweka rekodi zangu mbalimbali ambazo zitakuwa ngumu kuvunjwa,” alisema Manula.

SOMA NA HII  SOKA LA ROBERTINHO SIO POA MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA

Rekodi zinaonyesha Manula ametwaa tuzo ya kipa bora katika misimu minne mfululizo katika Ligi Kuu Bara huku msimu wa 2018-19, ligi ilikuwa haina mzamini kwahiyo hafla ya utoaji wa tuzo haikufanyika pengine ingefanyika hiyo angetwaa kwa mara tano mfululizo kutokana na rekodi bora ambazo alikuwa nazo.

MASHABIKI RUKSA

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeiruhusu Simba kuingiza mashabiki 10,000 katika mechi yao na AS Vita.

Katika mechi yao iliyopita dhidi ya Al Merrikh, Simba ilizuiwa kuingiza mashabiki, ila safari hii CAF imelegeza na kuwapa ruksa, jambo lililowapa mzuka mashabiki kwa kuamini vibe lao litawavuruga wapinzani wao waliowanyuka kwao 1-0.