Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO…MGUNDA AFICHUA JAMBO SIMBA…MASTRAIKA WAWEKWA KITIMOTO…

KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO…MGUNDA AFICHUA JAMBO SIMBA…MASTRAIKA WAWEKWA KITIMOTO…

Habari za Simba

Baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ugenini dhidi ya Horoya FC ya Guinea, Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi kazi kubwa wanayoifanya kwa sasa ni kuwapa programu maalum washambuliaji wao kuelekea mechi zijazo za michuano hiyo.

Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Jean Baleke, Moses Phiri na John Bocco ambaye alikosa nafasi nyingi za wazi katika mchezo uliopita.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu, Mgunda alisema wameona madhaifu ya kikosi chao hasa safu yao ya ushambuliaji kwa kutokuwa makini na kukosa utulivu hivyo kuandaa programu maalum katika mazoezi.

Alisema katika programu hiyo ni pamoja na kuwajenga kisaikolojia wachezaji wao na anaimani kubwa ya kufanya vizuri katika michezo iliyosalia ukiwamo watakaocheza nyumbani dhidi ya Raja Casablanca Jumamosi.

“Ni mechi ngumu na ushindani mkubwa, ukizingatia tumetoka kupoteza, lakini tutakuwa nyumbani na tunahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo dhidi ya Raja Casablanca.

“Kwa washambuliaji wetu inawalazimu kuwa na umakini na utulivu kichwani ili kufikia malengo ya kukusanya pointi tatu kila mechi tutakayocheza nyumbani,” alisema Mgunda.

Alisema wamewasoma wapinzani wao katika mchezo uliopita walipocheza na Vipers ya Uganda katika mechi ya kwanza, kwa kuona ubora na madhaifu ya Raja Casablanca.

“Ni timu nzuri, lakini tunatarajia kupata matokeo mazuri katika ardhi ya nyumbani, ninaimani wachezaji wetu wako vizuri na tunaendelea na maandalizi katika mchezo wetu huo,” alisema Mgunda.

SOMA NA HII  KUMBE ILE ISHU YA BILIONEA WA CHELSEA KUPEWA SUMU AKIWA UKRAINE IKO HIVI AISEE....