Home CAF SIMBA MIKONONI MWA WAARABU, GOMES HANA MASHAKA

SIMBA MIKONONI MWA WAARABU, GOMES HANA MASHAKA


 MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba wanaweza kukutana na timu kutoka Uarabuni katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Droo ya michuano hiyo mikubwa Afrika imepangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu itakayochezeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

 

Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ikiwa kileleni ikiwa na pointi 13 ikiwa imeweka rekodi huku ikiruhusu mabao mawili pekee na kufunga tisa katika mechi sita ilizocheza.

 

Simba inaweza kukutana na moja kati ya hizi timu tatu ambazo ni CR Belouizdad, MC Alger zote za Algeria au Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, ambazo hizo zote zimemaliza michuano hiyo katika nafasi ya pili zikitoka kundi B, D na C.


Simba itaanzia ugenini katika mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya Mei 14-15, mwaka huu na itamalizia nyumbani katika mchezo wa pili.

 

Akizungumzia hilo Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amesema: “Sisi tupo vitani, hivyo ni lazima tupambane kuhakikisha tunashinda kwa timu yoyote tutakayokutana nayo.


“Ninashukuru tumemaliza salama michuano hii bila majeruhi yeyote na hivi sasa nguvu zetu tunazielekeza katika hatua ya fobo fainali tuliyofuzu,”.


Mchezo wa sita Simba ilifunga kwenye hatua ya makundi kwa kupoteza mbele ya Al Ahly ambayo nayo imetinga hatua ya robo fainali kwa kufungwa bao 1-0.

Kwenye mchezo huo mshambuliaji wake Meddie Kagere alianza kikosi cha kwanza na alimaliza dakika 90 huku Chris Mugalu yeye alianzia benchi.

SOMA NA HII  SIMBA MWENDO WA PASI BAO KWA SASA